Wednesday, June 27, 2018

Marco Asensio

Real Madrid inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, mwenye umri wa miaka 22, ili kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar,mwenye miaka 26, ambapo imesemekana kuwa klabu Liverpool ina nia ya kumsajili mchezaji huyo. 

Chelsea imewasilisha ombi la dau la £35m kumnunua beki wa Juventus Daniele Rugani, 23. Klabu hiyo inatumai kwamba raia huyo wa Italia atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mkufunzi Maurizio Sarri. (Evening Standard)

Marouane Fellaini

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini atatoa tangazo kuhusu hatma yake mnamo tarehe mosi mwezi Julai. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 hajakubaliana na masharti ya klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Manchester Evening News)
Jack Grealish, 22, yuko tayari kuondoka Aston Villa msimu huu ili kurudi katika ligi kuu ya Uingereza, huku Tottenham ikiongoza katika kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza (Mirror)
Sokratis Papastathopoulos

Arsenal inakaribia kumsaini beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, huku ikiendelea na mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu, 22. (Sky Sports)

Manchester United inamchunguza beki wa Itali na AC Milan Leonardo Bonucci, 31. (Yahoo)
Aaron Mooy

Manchester City inatazama uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Australia Aaron Mooy, 27, kutoka Huddersfield . City pia ina mpango wa dau la £20m huku Everton, West Ham United na Southampton pia wakipanga kumnunua Mooy. (ESPN)
Divock Origi
Liverpool itamchunguza mshambuliaji wake wa Ubelgiji Divock Origi ,23, katika kipindi cha wiki chache zijazo na kumpatia fursa kuonyesha umahiiri wake katika klabu hiyo. Origi alihudumu msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika klabu ya Wolfsburg Ujerumani. (Liverpool Echo)

Wolves wamekataa ombi la dau la £12m kwa mshambuliaji wa Fulham na raia wa Ureno Ivan Cavaleiro, 24, (Sky Sports)
Craig Dawson

West Brom haimtaruhusu beki wa Uingereza Craig Dawson kuondoka katika klabu hiyo kwa gharama ya chini. Klabu hiyo ilikataa dau la £12m kutoka West Ham kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Stoke City wanakaribia kuweka mkataba na winga wa West Brom na Jamhuri ya Ireland James McClean, 29, baada ya kuimarisha dau la kwanza la £4m bid. (Mail)
Marcelo Bielsa
Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumsaidia Marcelo Bielsa katika klabu ya Leeds kumpatia baadhi ya wachezaji wake kwa mkopo . (Sun)

Sporting Lisbon itamfuta kazi mkufunzi wake Sinisa Mihajlovic, siku chache tu baada ya kuajiriwa.(Record)

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video