Wednesday, June 27, 2018

Baada ya kuwaliza mbele ya mashabiki wa nyumbani wakiwa wenyeji wa Kombe la Dunia 2002, Ujerumani nayo imepata kuhisi uchungu wa kutolewa Kombe la Dunia.

Mabao ya Son Heung-min dakika ya 96 na Kim Young-gwon dakika ya 91 yametosha kuidhalilisha Ujerumani na kuitema kutoka Dimba la Dunia.

Aidha, Ujerumani yenye mazoea ya kuwadunisha wengine, imeadhibiwa pia kufuatia unyama iliyowatendea Brazil 2014 kwa kuwafunga 7-1 mbele ya mashabiki wa nyumbani.
Ujerumani imejiunga na Ufaransa, Italia na Uhispania kuwa mabingwa waliochujwa kutoka taji walicholenga kulitetea.

Die Mannschaft waliingia mchuano huo ukiwa wa mwisho, wakipigiwa upatu kwa kuwa na nafasi nzuri ya kufuzu kutoka hatua ya makundi.

Korea Kusini imekuwa taifa la kwanza kutoka bara Asia Kuifunga Ujerumani.
Licha ya matokeo hayo, Korea Kusini na Ujerumani wameelekea nyumbani huku Sweden na Mexico wakielekea hatua ya mchujo.

Sweden iliyomaliza wa kwanza Kundi F, inamsubiri wa pili katika Kundi E kati ya Uswizi na Brazil.
Mexico itakuwa na kibarua kwani itachuana na kiongozi wa Kundi E wakisaka nafasi ya kushiriki hatua ya Robo fainali.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video