Tuesday, June 26, 2018

Mchezaji wa klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Argentina Marcos Rojo na Lionel Messi wa klabu ya Fc Barcelona wakishangilia bao la ushindi walilolipata dhidi ya timu ya Taifa ya Nigeria.

Mkwaju wa Marcos Rojo katika dakika za majeruhi ndiyo ulioziumiza roho za waafrika wengi na kupeleka furaha kwa wa Argentina wakivuka kwa shangwe kuelekea katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la 2018.

Kama si mlinzi wa Manchester United Rojo kusogea katika eneo la hatari la Nigeria na kuipokea mpira uliopigwa na Gabriel Mercado, Argentina ilikuwa hoi kuelekea kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa ya mpira wa miguu Duniani.

Lionel Messi ambaye alikuwa amefunga goli safi la kwanza, alimrukia Roho mgongoni kwa furaha, wakiungana na wenzao waliokuwa kwenye benchi la ufundi katika kushangilia ushindi.

Yalikuwa matokeo waliyostahili baada ya kuwa wamecheza vibaya katika kipindi cha pili kiasi cha kosa lililofanywa na Javier Mascherano kusababisha Nigeria kusawazisha kupitia mkwaju wa penati uliotiwa kimiani na Victor Moses anayechezea klabu ya Chelsea ya England.
Nahodha wa Argentina Lionel Messi ambaye katika mechi hii alikuwa na jukumu la ziada kama kiongozi kutokana na mgogoro uliopo kati ya wachezaji na mwalimu Jorge Sampaol, amesema, "Ninawashukuru watu wote walioko hapa, kwa kujitolea kwao, na wale walioko nyumbani Argentina ambao muda wote walikuwa nasi"
Naye nahodha wa Nigeria John Obi Mikel amesema, " Tumefanya kila tuliloliweza.

Katika kipindi cha pili tumepambana na kupambana. Basi tu haikuwa. Hii ni timu changa na katika miaka minne ijayo wengi wao watakuwa tayari kwa michuano hii".Ninajivunia vijana hawa na tulichokifikia. Nadhani tumefanya vizuri sana. Tunapaswa kusonga mbele"

Messi anakuwa mchezaji wa tatu wa Argentina kuwahi kufunga katika michuano mitatu ya Kombe la Dunia (2006, 2014 na 2018) baada ya Diego Maradona (1982, 1986 na 1994) na Gabriel Batistuta (1994, 1998 na 2002).
Nusu ya idadi ya magoli yake 6 ya Kombe la Dunia, ameifunga Nigeria.

Bila shaka baada ya mchezo huu, mambo mawili yataendelea kuwa gumzo ni pamoja na afya ya afya ya Diego Maradona ambaye pamoja na vibweka kadhaa uwanjani, inadaiwa amekimbizwa hospitali mara ya mchezo.

Jambo la pili la kimjadala itakuwa ni kuhusiana na iwapo Nigeria walistahili kupata Penalti wakati Rojo alipoupiga kwa kichwa mpira na mpira huo ukamgusa mgono kabla ya mwamuzi Cuneyt Cakir kwa msaada wa teknolojia ya video kuamua kuwa siyo penati.

Sasa Argentina watakutana na mshindi wa kundi C, Ufaransa, wakati mshindi wa kundi D Croatia ambaye ameishikilia nafasi ya kwanza baada ya kuwabamiza Iceland 2-1, akikwaana na Denmark.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video