VPL LEO: NDANDA FC YAICHAPA RUVU SHOOTING NANGWANDA SIJAONA
LIGI Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) imeendelea leo kwa Mchezo mmoja kuchezwa katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona Mkoani Mtwara ambapo Wenyeji Ndanda FC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Maafande wa Ruvu Shooting.
Bao pekee la Ushindi kwa Wana 'Mtwara Kuchele' Ndanda FC limefungwa na Mshambuliaji wao hatari, Omary Mponda.
Hilo ni goli la 6 kwake Msimu huu wa VPL.
0 comments:
Post a Comment