SIMBA SPORTS CLUB
Dar es salaam, Tanzania
6/3/2017.
Dar es salaam, Tanzania
6/3/2017.
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.*
Vinara wa ligi kuu Tanzania Bara, Klabu ya Simba imekubali
mwaliko wa Chama cha mpira wa miguu mkoani Dodoma (DOREFA) Kwa ajili ya
kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Polisi ya mjini humo siku
ya Jumamosi hii tarehe 11-3-2017.
Kwa kuwa klabu yetu haitakuwa na mchezo wa ligi kuu
wikiendi ijayo, tunaamini washabiki wetu wa Dodoma na mikoa ya jirani
watapata fursa adhimu ya kuiona ya klabu yao. Pia tunatarajia kuutumia
mchezo huo Kama maandalizi ya mechi yetu ya Kombe la Shirikisho hatua ya
Robo fainali itakaochezwa machi 18.
Tunaamini pia buradani hiyo *MUBASHARA,* wataipata pia
watumishi wa umma ambao wameshaanza kuhamia Makao makuu ya nchi
kutekeleza agizo la Mh Rais wa Jamhuri *Dr John Pombe Magufuli*
Imetolewa na
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI NA MAWASILIANO SIMBA SC.
MKUU WA HABARI NA MAWASILIANO SIMBA SC.
*SIMBA NGUVU MOJA*
0 comments:
Post a Comment