
Vinara wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (VPL) Simba wataanzia ugenini Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Mjini Arusha wakicheza na Wenyeji Madini FC.
Yanga au Kiluvya United zinazokutana kesho Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kwenye mechi ya Mwisho ya Raundi ya 16, yoyote itakayeshinda atakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons na haijapangiwa tarehe.
Ratiba kamili iko kama ifuatavyo:
Machi 18, 2017
Kagera Sugar vs Mbao FC-Uwanja wa Kaitaba, Kagera
Madini FC vs Simba SC-Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha
Azam FC watakuwa wenyeji wa Ndanda FC Dimba la Azam Complex, Dar es Salaam, lakini mechi hiyo haijapangiwa tarehe kwasababu Azam FC watakuwa na majukumu ya kuiwakilisha Tanzania katika Mashindano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment