Tuesday, February 7, 2017

Kikosi cha Simba, kimeendelea na mazoezi yake kujiandaa na mechi yao dhidi ya Tanzania Prisons ya Mbeya itayochezwa Jumamosi hii Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam.
Simba imefanya mazoezi chini ya Kocha Joseph Omog akisaidiana na msaidizi wake, Jackson Mayanja ambao kwa pamoja wameonesha kubadilika kwa kuifanya timu yao icheze kwa kushambulia zaidi.
Mazoezi ya Simba yamefanyika kwenye Uwanja wa Polisi Kilwa Road jijini Dar.
Katika mechi iliyopita, Simba iliitwanga Majimaji FC kwao Songea kwa mabao 3-0, ambayo yalifungwa Ibrahim Ajib, Said Ndemla na Laudit Mavugo.
Kwa kufunga siku hiyo, Ajib alifikisha mabao manne msimu huu wa VPL, huku Mavugo akifikisha mabao matano na Ndemla lilikuwa bao lake la kwanza.
Kabla Simba ilikuwa ikishinda kwa tofauti ya bao moja huku kikosi kikionesha kujilinda zaidi, lakini kwenye mechi dhidi ya Majimaji, ilikuwa ikipeleka mashambulizi mengi zaidi.
Simba kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo ikiwa na alama 48 nyuma ya Yanga wanaoshikilia usukani kwa pointi 49, huku timu zote zikishuka dimbani mara 21.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video