Monday, January 30, 2017

TANZIA: Habari zilizotufikia MPENJA SPORTS zilizothibitishwa zinasema, David Buruhan Golikipa wa Kagera Sugar na mtoto wa Mshambuliaji wa zamani wa PAN Abdallah Buruhan amefariki leo Hospital ya Bugando Mwanza.
Ripoti za awali zinaeleza kwamba Mlindamlango huyo Aliumwa ghafla wakiwa njiani kuelekea Singida kwenye mechi ya Azam Federation Cup na waliporudi Kagera hali yake ikazidi kuwa mbaya na hivyo kukimbizwa Bugando.
Hii ni kwa mujibu wa Kocha wake Mecky aliyenipigia asubuhi hii na leo Jioni kocha huyo anategemea kuiongozo Kagera Sugar dhidi ya Waajiri wake wa zamani, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.
Enzi za uhai wake, Buruhani aliwahi kuidakia kwa Mafanikio Mbeya City na Majimaji FC.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video