Ligi kuu soka Tanzania Bara
inaendelea kesho kwa mechi moja kuchezwa Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam
kati ya African Lyon dhidi ya mabingwa watetezi Yanga.
African Lyon
wataingia katika mchezo wa kesho wakiwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu na Azam
FC kwenye mechi ya Jumapili iliyopita Uwanja wa Uhuru, wakati Yanga wao
walishinda mabao matatu kwa bila dhidi ya JKT Ruvu.
Ugumu wa
mechi ya African Lyon na Yanga unatokana na mazingira ya timu zote mbili kwenye
msimamo wa Ligi kuu ambapo Yanga wapo katika mbio za Ubingwa wakizidiwa pointi
mbili na vinara Simba wanaoongoza kwa pointi 38 baada ya timu zote kushuka
dimbani mara 16.
African Lyon
wao wapo kwenye harakati za kukwepa kushuka daraja wakiwa nafasi ya 12 kwenye
msimamo wa VPL wakijikusanyia kibindoni pointi 18 katika mechi 16 walizoshuka
dimbani .
Hata hivyo
Yanga wamekuwa na rekodi nzuri dhidi ya African Lyon kwani hata mechi ya
mzunguko wa kwanza iliyochezwa Agosti 28 mwaka huu, Yanga waliibuka na ushindi
wa mabao matatu kwa bila.
Mabao ya
Yanga kwenye mchezo huo yalifungwa na Deus Kaseke, Simon Msuva na Juma Mahadhi.
Mechi
nyingine sita za VPL zitachezwa Jumamosi hii kwa Mbeya City, Wanakoma Kumwanya
kuwa wenyeji wa Toto African Wanakisha Mapanda katika Uwanja wa Sokoine, Jijini
Mbeya.
Wana
Supankurukumbi Kagera Sugar watakuwa dimbani kwao Kaitaba kuwakabili Stand
United, Chama la Wana.
Huko
Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, Ndanda FC, watapepetana na Kagera Sugar, huku
Nyasi bandia za Uwanja wa Uhuru zikiwaka moto kwa vinara Simba kukabiliana na
Maafande wa JKT Ruvu Stars.
Majimaji
Wanalizombe watakuwa wenyeji wa Azam FC uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma,
wakati Matajiri wa madini ya Almasi, Mwadui FC watawaalika Mbao FC kwenye
uwanja wa Mwadui, mkoani Shinyanga.
Mzunguko huo
wa 17 wa VPL utamalizika Boxing day Jumatatu ya Juma lijalo kwa Ruvu Shooting
kucheza na Tanzania Prisons Uwanja wa Mabatini Pwani.
0 comments:
Post a Comment