Klabu ya
Chapecoense ya Brazil ambayo hivi karibuni ilipoteza takribani kikosi kizima
kutokana na ajali ya ndege iliyotokea karibu na mji wa Medellin nchini
Colombia, rasmi imekabidhiwa kikombe cha ubingwa wa Sudamericana.
Itakumbukwa
kikosi hicho kilikuwa kikielekea nchini Colombia kwaajili ya mchezo wake wa
mwisho wa fainali ya klabu bingwa ukanda wa America ya Kusini dhidi ya wenyeji
Atletico Nacional kabla ya kukumbwa na msiba huo mzito.
Wapinzani
wao kwa kushirikiana na waandaji waliamua kuwakabidhi ubingwa huo kama sehemu
ya kuomboleza kile kilichowakuta na hatimaye wapewa ubingwa wao wakati wa droo
ya pangazi wa michuano ya msimu ujao.
Chapecoense
imepangwa kundi moja na Club Nacional ya Uruguay, Zulia ya Venezuela na Lanus
ya Argentina.
Kikosi hicho
kitashuka kwa mara ya kwanza dimbani tangu kutokea kwa ajali hiyo Januari 29
mwakani ikiwa ni siku nne tu baada ya Brazil kucheza mchezo wa kimataifa wa
kirafiki dhidi ya Colombia mjini Rio, lengo la mchezo huo ni kukusanya fedha
kwaajili ya kuichangia Chapecoense.
0 comments:
Post a Comment