Shirikisho
la Soka nchini TFF limeanza kufikiria kubadili tarehe ya mchezo wa mzunguko wa
pili wa ligi kuu soka Tanzania Bara VPL kati ya watani wa jadi Simba na Yanga
maarufu kama Dabi ya Kariakoo ambao umepangwa kufanyika Februari 18 mwakani.
Hatua hii
imetokana na siku hiyo kuingiliana na mechi ya marudiano ya raundi ya awali ya
ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo wawakilishi wa Tanzania Yanga watachuana ugenini
na Ngaya FC ya Comoro.
Mkurugenzi
wa Mashindano wa TFF, JONAS KIWIA amethibitisha kwamba kutokana na muungiliano
wa ratiba hiyo ya CAF, hawana jinsi zaidi ya kupangua mchezo huo wa VPL.
Kwa mujibu
wa Droo ya CAF ya Ligi ya mabingwa Afrika iliyotolewa jana, Yanga watacheza
mechi ya kwanza ya raundi ya awali kati ya Februari 10, 11 au 12 Uwanja wa
Taifa jijini Dar es salaam ambapo wameingia mkataba na serikali juu ya kutumia
uwanja huo kwenye mashindano ya CAF, wakati mechi ya marudiano inatarajiwa kuwa
kati ya Februari 17, 18 au 19 nchini Comoro.
0 comments:
Post a Comment