Chama cha soka cha Afrika kusini
(SAFA) kimemtimua Ephraim 'Shakes' Mashaba aliyekuwa akiinoa Bafana Bafana na
kuahidi kumchukulia hatua za kinidhamu kocha huyo mwenye miaka 66.
Kibarua cha
Shakes Mashaba kilionekana kipo mashakani baada ya kuwatolea mbovu waajiri wake
wakati kikosi chake kilipopata ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Senegal katika
mchezo wa kuwania kufuzu fainali zijazo za kombe la dunia mwezi uliopita.
Aliadhibiwa
kwa kuodolewa kwenye orodha ya msafara wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini
uliokwenda mjini Maputo na kuanzia hapo alikuwa na wakati mgumu wa kutetea
ugali wake.
Mashaba
aliiongoza Bafana Bafana katika AFCON ya mwaka 2015 lakini mafanikio hayo
yaliingiwa na shubiri baada ya kushindwa kuipeleka Gabon kwenye za kombe la
mataifa ya Afrika mwezi Januari mwakani.
SAFA imetoa
tamko rasmi la kuachana na Kocha huyo ambae amepelekwa katika kamati ya nidhamu
iliyosikiliza shauri lake kwa muda wa siku tano mwezi huu lililoongozwa na
mtaalamu huru wa masuala ya sheria anaefanya kazi za uwakili kwenye mahakama
kuu.
Baada ya
kuhitimisha shauri hiyo Mwenyekiti wa kikao alitangaza kumtia hatiani kocha
huyo kwa mambo makubwa matatu.
Jambo la
Kwanza na la pili, amekiuka ufanisi wa kazi yake kama mkufunzi mwenye taaluma
na jambo la tatu amevunja taratibu za mawasiliano za SAFA.
Mtendaji
mkuu wa Chama hicho Dennis Mumble amesema chama cha chake kitaanza mchakato wa
kumtafuta mrithi wa Mashaba hivi karibuni na moja ya kigezo muhimu, kocha huyo
anapaswa kuwa na ufahamu na soka la barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment