Klabu ya
Crystal Palace imeachana na Kocha mkufunzi wake Alan Pardew kufuatia mwenendo
mbovu walio nao msimu huu wa ligi kuu ya England.
Crystal Palace ipo katika nafasi ya 17 ikiwa
na alama 15 ambapo wameshinda mechi nne, wametoka sare mechi tatu na kupoteza
mechi 17.
Alan Pardew aliteuliwa
kukinoa kikosi hicho mwezi Januari mwaka jana kwa mkataba wa miaka mitatu na
nusu hata hivyo ushindi wa mechi moja kati ya 11 ni miongoni mwa sababu
zilizofupisha ajira yake.
0 comments:
Post a Comment