Waandaaji wa
Olympic ya Tokoyo mwaka 2020 wamewasilisha mapitio ya bajeti ya michezo hiyo
ambayo imeonekana kuwa na mapungufu makubwa ya gharama za matumizi.
Kutoka Dola
za kimarekani Billion 17 bajeti mpya iliyowasilishwa ni kati ya Dola Billion 13
hadi 15 ambazo ni zaidi ya Shilingi Trilioni 36 za kitanzania.
Waandaaji
mji wa Tokyo wamekutana na Serikali ya mji huo, uongozi wa kitaifa wamekutana
kupitia tena punguzo la gharama ambalo wameahidi kufanya kila linawezekana ili
kuipunguza zaidi na kufanikisha michezo hiyo kufana ikilinganishwa na Olimpiki
ya Rio mwaka 2016.
Mgawanyo wa
matumizi Dola Billion 5 nukta tano zitatumika kujenga viwanja vya muda na
miundombinu mingine, Dola Billion 3 nukta nane kwaajili ya gharama za usafiri
na ulinzi.
0 comments:
Post a Comment