
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa viwango vya ubora wa vilabu barani Africa na Mabingwa watetezi Yanga wameongoza kwa timu za Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania Yanga SC imeshika nafasi ya 331 mbele ya Azam FC iliyo katika nafasi ya 351, wakati mahasimu wao wakubwa timu ya Simba wanashika katika nafasi ya 356 huku timu za kiarabu zikitesa.
Yanga wamepata pointi nyingi kutokana na ushiriki wao katika michuano ya CAF wakivuka raundi ya pili klabu bingwa Afrika msimu wa 2015-16 na kufika hatua ya nane bora kombe la Shirikisho.
Uongozi wa Yanga SC umefurahia takwimu hizi lakini wakijinadi kujipanga vyema ili michuano ya klabu bingwa iliyo mbele yao iwafikishe ndani ya 100 bora ya Afrika lakini wakiweka mkakati zaidi kushika namba moja ya Afrika.
Pongezi nyingi ni kwa mwalimu Hans Van Pluijm na wenzake wote wa benchi la ufundi ambao walipambana vyema kuhakikisha timu inasonga mbele katika michuano hiyo.
" Yanga ni moja timu kubwa Afrika kwa miaka iliyonayo hivyo inahitaji maendeleo makubwa kimbinu na kiufundi . Nimefurahi rekodi hii kuwa bora juu ya vilabu vingine Tanzania lakini bado si mafanikio stahiki kwa klabu hii . Inahitaji kuwa ndani ya 100 bora za Afrika au 50 "
Hiyo ni kauli ya Hans Van Pluijm akihojiwa na idara ya habari ya Yanga SC .
0 comments:
Post a Comment