Friday, November 25, 2016

Kiungo mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Anderson alirusha kijembe kwa nahodha wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard siku moja tu kabla ya kutangaza kustaafu rasmi kucheza soka.

Gerrard (36) anakuwa moja ya wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea Liverpool baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa klabuni hapo, ikiwa ni pamoja na kushinda taji la Champions League na mataji mawili ya FA.

Hata hivyo, Gerrard hajawahi kushinda taji la Premier League na, akiongea kabla ya kutangaza kustaafu, Anderson ametanabaisha kwamba ameshinda mataji mengi zaidi kuliko nahodha huyo wa zamani wa England.

"Nimeshinda kila kitu kwenye klabu. Nimeshinda mataji manne ya Premier League," alisema. "Mchezaji kama Gerrard, ambaye ameichezea Liverpool, mchezaji ambaye ana historia kubwa katika ulimwengu wa soka, hajawahi kushinda taji hilo hata mara moja. Wakati mimi nimeshinda mara nne.

“Nimeshinda Kombe la Dunia ngazi ya klabu. Vilevile Champions League. Nimecheza tatu fainali za Champions League.

"Nilipowasili klabuni pale, wachezaji wote walinifurahia. Mara nyingi walikuwa wakitaniana. Walikuwa wacheshi kwa kweli. Naweza kusema Manchester United ndio klabu namba moja kwangu ulimwenguni kote."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video