Sunday, November 27, 2016

Ni jambo la kushangaza kidogo. Licha ya kutawala La Liga kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kushinda mara kadhaa katika Uwanja wa Santiago Bernabeu, Mestalla na viwanja vingine, Barcelona wameshindwa kunusa ushindi kwenye Uwanja wa Anoeta tangu mwaka 2007.

Ushindi wa mwisho kwa Barca ugenini dhidi ya Real Sociedad ulikuwa ni Mei 5 mwaka 2007. Wakati huo, Frank Rijkaard  akiwa kocha mkuu na kipindi hicho Barca walikuwa wakiwania kushinda taji la La Liga kwa mara ya tatu mfululizo, kabla ya kushindwa na Real Madrid kutokana na rekodi yao mbovu ya head-to-head.

Claudio Bravo alikuwa langoni mwa wakali hao wa Basque wakati Andres Iniesta na Samuel Eto'o walifunga magoli kwa upande wa Barca ambapo Lionel Messi pia alikuwepo. Real Sociedad walishuka daraja msimu huo, lakini tangu waliporejea La Liga kwa mara nyingine mwaka 2010, wamekuwa ni mwiba mkali kwa Barcelona kwenye dimba la Anoeta. 

Sociedad walishinda mabao 2-1 mwishoni mwa msimu wa 2010-11. Msimu wa 2012-13 walishinda mabao 3-2 wakati huo Barcelona ikiwa chini ya Tito Vilannova, baadaye wakipa kipigo Barca ya Tata Martino magoli 3-1 msimu wa 2013-14, kabla ya kumwashia moto Luis Enrique kwa kumfunga bao 1 kwa misimu miwili mfululizo. Walitoka sare ya bao 1-1 Anoeta kwenye mchezo wa Copa del Rey mwaka 2014.

Msimu wa 2010-11, Barca walikwenda Anoeta wakiwa mbele kwa alama tisa wakati huohuo wakikabiliwa na kibarua kigumu cha nusu fainali ya Champions League dhidi ya mahasimu wao Real Madrid. Pep Guardiola alichagua kikosi dhaifu kikjumuisha wachezaji kama Jose Pinto, Andreu Fontas, Martin Montoya, Jeffren na Ibrahim Afellay na kuambulia kichapo.

Anoeta ni uwanja rafiki kwa timu ngeni zinazokuja kucheza kwasababu kuna running track uwanjani hapo ambazo zinasaidia mashabiki kuwa mbali na sehemu ya kuchezea ukilinganisha na viwanja vingine. Hata hivyo, wakali hao maarufu kwa jina la Basques wamekuwa akijivunia rekodi zao dhidi ya mechi kubwa wanazocheza uwanjani hapo wakiamini ndiyo wakati wa kuonesha ubora wao. Kwa miaka ya hivi karibuni, Real Sociedad wamekuwa wakiwa na option kubwa ya mbinu za kiuchezaji hasa wakiwekeza kwenye matumizi ya nguvu, suala ambalo Barca linawapa taabu hasa wanapopmbana na timu zinapendelea matumizi ya nguvu.

Kuhusu dhana ya Barcelona kuwa na laana kwenye dimba hilo la Anoeta si kweli, kwasababu imeshawahi pia kutokea kwa Real Madrid kudumu kwa zaidi ya miaka 18 bila ya kuonja ladha ya ushindi dhidi ya Deportivo La Coruna kati ya mwaka 1991 na 2010. Wakati mwingine, masuala kama haya hutokea na hukaa akilini mwa wachezaji kitu kinachopelekea hali hiyo kuendelea kudumu.

Kitu pekee kitakachopelekea Barca kumaliza mkosi huo ni kutoangalia matokeo ya nyuma badala yake wacheze kwa kujituma ili kupata ushindi kama kocha wao alivyonukuliwa akisema: "Hatutaenda kucheza pale tukiangalia historia ya nyuma kwa kuwa huu ni mchezo mwingine."

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video