Monday, November 28, 2016

Manchester United wamekuwa katika wakati mgumu kunako Ligi ya England kutokana na matokeo yasiyoridhisha hasa kutokana na ukubwa na hadhi ya klabu ya hiyo. Mourinho amepoteza kujiamini na kuamini timu yake...kwanini? Unakumbuka kuelekea mchezo wa jana alisemaje? Alisema: "Nilisema kabla ya mchezo dhidi ya Arsenal kwamba sikuwa nikifirikia kama kuna miujiza yoyote ingetokea kwenye mchezo ule, lakini sikuwa sahihi japokuwa hisia zangu hazijabadilika. Kama tukicheza kwa kiwango kile dhidi ya Arsenal basi tutashinda. Kama tutajikita kucheza vizuri basi vijana wangu watapata watakachostahili."

Jana kwa mara nyingine tena Manchester United walicheza mpira mwingi mno na kupata umiliki mkubwa, zaidi ya hapo walitenegeneza nafasi za kutosha lakini walishindwa kupata matokeo mbele ya Wagonga Nyundo wa London West Ham United. Sare ya 1-1 kwenye dimba la Old Trafford maana yake wameshindwa kupata ushindi kwenye michezo ya ligi kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu September 24, wakati walipowafunga mabingwa watetezi Leicester City.

Uwepo wa Zlatan Ibrahimovic, Jesse Lingard, Paul Pogba, Juan Mata, Marcus Rashford, Henrikh Mkhitaryan na Wayne Rooney hakufua dafu mbele ya West Ham.

Kila kitu kilikuwa upande wao, lakini save za kipa wa West Ham Darren Randolph kutoka kwa Rashford, Rooney na Pogba na Lingard zilikuwa mwiba mchungu kwa Manchester United.

United walitakiwa kuongeza juhudi japo kidogo ili kupata goli la ushindi baada ya Ibrahimovic kusawazisha goli la mapema la Diafra Sakho. Hakuna kitu cha zaidi ambacho Mourinho angeweza kuwaambia wachezaji wake kufanya zaidi ya walichofanya jana.

Hakuwa kwenye jukwaa kwenye kipindi chote cha pili baada ya kupewa amri na mwamuzi Jonathan Moss aondoke kwenye benchi na kwenda kukaa jukwaani baada ya kupiga kopo la maji kwa hasira akimtuhumu mwamuzi kumpa kadi Pogba kwa kujiangusha, hivyo kukosa nafasi ya kuwapa maelekezo zaidi wachezaji wake.

Matokeo hayo sasa yanawafanya kuwa nyuma kwa alama 11 nyuma ya vinara wa ligi hiyo na alama 8 nyuma ya timu inayoshika nafasi ya nne 

Kwa mtazamo wa kawaida licha ya kuwa katika hali ile ile kwa wakati huu kama ilivyokuwa misimu kadhaa iliyopita, Man United ya Mourinho inaonekana kuwa bora zaidi ya ile ya David Moyes na Louis van Gaal. 

Lakini kitu ambacho Mourinho anapaswa kufanya ni kuondokana na dhana ya timu yake kuonewa na kupambana kuondokana na upepo mbaya ili timu iweze kurejea katika hadhi yake kama ilivyokuwa wakati wa Sir Alex Ferguson.

Asipende kufanya mambao ya kitoto na yasio na manufaa, hali inayopelekea kuigharimu timu yake kucheza bila ya kocha wao badala yake anapaswa kuamini waamuzi ni weledi na maamuzi yao yanapaswa kuheshimiwa.

Ni timu nyingi sana ambazo zimekuwa zikifanyiwa maamuzi ambayo hayaendi upande wao lakini makocha wao hawafanyi anayofanya Mourinho. Hivyo ifikie wakati Mourinho aachane na tabia zisizo za kimichezo na afanye kazi kwa kuisaidia klabu yake na si vinginevyo.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video