Monday, July 25, 2016

Beki wa Arsenal Per Mertesacker anaamini ilikuwa ni miujiza kwa timu yake kushika nafasi ya pili katika msimu uliopita wa ligi ya England.
Arsenal waliwapiku mahasimu wao wa jiji la London Tottenham na kushika nafasi ya pili katika siku ya mwisho kabisa ya msimu, japokuwa walimaliza alama 10 nyuma ya vinara na mabingwa Leicester City.
Na Mertesacker, ambaye anataraji kutangazwa kuwa nahodha mpya wa timu kufuatia kustaafu kwa Mikel Arteta anaamini kwamba Arsenal walikuwa na bahati kubwa.
"Kwa namna ambavyo msimu uliopita ulienda, tulikuwa ni wenye bahati kubwa kumaliza nafasi ya pili," aliliambia gazeti la The Sun
"Mambo yalibadilika siku ya mwisho na hali hiyo ikawa kama kiujiza kwetu kumaliza nafasi ya pili."
"Kilichotufedhehesha ni kwamba Leicester walitumia vizuri sana udhaifu wa vilabu vikubwa kujichukulia pointi lakini sisi tulishindwa."
Huku zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya kuanza kwa msimu mpya, Arsenal mpaka sasa wamesajili mchezaji mmoja tu mwenye jina kubwa ambaye ni Granit Xhaka kabla ya kukutana na Liverpool August 14.
Na Mertesacker anaamini kwamba usajili uliofanywa na wainzani wao utaleta uumu mkubwa kuelekea msimu mpya wa ligi hasa kwa timu yake ya Arsenal.
"Hii itakuwa changamoto kubwa kwetu, kuhakikisha tunapambana na timu zote bora ambazo zilimaliza nyuma yetu," aliongeza.
"Bila shaka, timu hizo kubwa zitakuwa imara zaidi msimu huu. Hicho ndivyo tunavyotaraji kuona msimu mpya utakapoanza huku kukiwa na wachezaji wengi wapya.
"Usajili mwingi umefanyika, na kamwe haitaokuwa rahisi kwetu msimu huu, hasa kutokana na usajili uliofanywa na wenzetu."

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video