
Kama ilivyoada kwa Jose Mourinho, mara nyingi amekuwa ni mtu wa kufanya mambo ambayo muda mwingi yatawaacha watu wakimzungumzia. Kwa sasa yupo nchini China kwa ajili ya michezo ya maandalizi kuelekea msimu mpya wa ligi na michuano mingine.
Kulekea mchezo wao wa nternational Champions Cup ambao ulitakiwa kufanyika leo dhidi ya Manchester City na kuahirishwa kutokana na sababu za hali ya hewa, Mourinho aliamua kupanga upya mkutano wake na waandishi wa habari huku kukiwa hakuna sababu yoyote ya msingi. Lengo likiwa na kupata media nyingi zaidi za kumpa 'headline'.
Pep Guardiola kwa upande wake hakujali kwamba mkutano wake wa awali dhidi ya wanahabari ulihudhuriwa na watu wachache. Ni mtu ambaye anaonekana kutotaka kuendeleza malumbano ya enzi za Real Madrid na Barcelona.
Tuachane na hayo....kikubwa ni kwamba wawili hawa wanajikuta wakikutana mapema zaidi kuliko hata walivyodhani.
Lakini pengine Mourinho na Guardiola wanaweza kufurahishwa na jambo hili la wao kukutana mapema, kwa sababu ni kipimo tosha cha kujaribu kutathmini uwezo wa wachezaji wao uliofikia mpaka sasa.
Kwa timu zote yaani United na City ambazo zlikuwa zikutane leo kuwania kombe hili la International Champions Cup, ni fursa kubwa kwao kuona kama wiki tatu zilizosalia kabla ya msimu mpya wa ligi kuanza, je, vijana wao watakuwa katika hali gani.
United waliwafunga Wigan katika mchezo wao wa awali wa kirafiki lakini walipokea kipigo kitakatifi magaoli 4-1 kutoka kwa Borussia Dortmund Ijumaa iliyopita.
Katika mchezo huo mengi yalielezwa kutokana na ukweli kwamba Dortmund tayari wameshacheza mechi nyingi zaidi za kirafiki kabla ya kukutana na United, kwa maana ya kwamba walikuwa fiti zaidi kuelekea kwenye mchezo ule.
Lakini ni ukweli ulio wazi kwamba, Wajerumani hao wamekuwa wakicheza soka lenye mvuto na mafanikio kwa miaka kadhaa sasa, na walionekana kama watu ambao walikuwa wanajua nini wanatafuta kuelekea mchezo ule. Kitimu na mchezaji mmoja-mmoja walikuwa bora kuliko United.
Kwa kipindi cha miaka miwili hivi, Louis van Gaal alipandikiza falsafa ambayo ilikuwa tofauti kabisa na ile iliyozoeleka. Kwenye mchezo ule wachezaji wengi walikuwa wako taratibu na wanatabirika kwa kile wanachotaka kufanya.
Mourinho anahitaji muda kufanya mabadiliko kutokana na namna ambavyo timu yake ilikuwa ikipambana na Dortmund, na hali ile imemkumbusha ni kwa kisai gani ana kazi kubwa ya kufanya klabuni hapo, licha kwamba siku ile hakuwa na wachezaji wake muhimu kama Wayne Rooney, Chris Smalling na Anthony Martial.
Fursa hii ya kukutana na vijana wa Guardiola, basi inawezekana ikawa imekuja kwa wakati sahihi hata kama wote wako kwenye uwanja wa ugenini.
Man City kwa upande wao, mpaka sasa wamecheza mchezo mmoja tu wa kirafiki huku wakipambana kuendana na mfumo mpya wa kocha wao mpya. Mfumo wenye asili ya Kikatalunya unaotaka umiliki mkubwa wa mpira unaotokana na kupiga pasi nyingi.
Bayern Munich walimpa upinzani mkubwa Guardiola kwenye mchezo wake wa kwanza wa kirafiki, na hii ilitokana na ukweli kwamba wachezaji wa Bayern bado walikuwa na fikra za mfumo wa kocha huyo kufutia kukaa na Ancelotti kwa muda mfupi tu. Wakati zikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya kuanza kwa ligi, Guardiola alishahadharisha kwamba anahitaji kupewa muda ili kufanya makubwa klabuni hapo.
Mourinho alioneka kuzungumza kimashihara kuwalelezea Dortmund kabla ya mchezo wao wa Ijumaa, huku Guardiola jana akisema kwamba mpaka sasa ameitazama United kidogo sana. Kwa hatua kama hii, ushindi si muhimu sana. Hata kama ni mchezo ambao unawakutanisha mahasimu wawili wa England.
Huu ni mchezo muafaka kwa wawili hao wa jiji la Manchester kupata somo juu ya wao wenyewe na vile vile japo kidogo kufahamiana kwa uzuri juu ya mbinu mpya za makocha wapya.
Licha kwamba Leicester walikuwa bora msimu uliopita, lakini kuna kila dalili kwamba haitakuwa rahisi kwao kurudia kile walichokifanya msimu uliopita, kutokana na miamba ya ligi hiyo kupambana kurudi kwenye nafasi zao walizozoea kuwa.
Wote kwa pamoja Mourinho na Guardiola wameletwa na vilabu vyao kwa sababu ya kuvirudisha katika zama zao. Kuna dhana ama fikra kwamba mmoja wa makocha hawa aliajiriwa kutokana na uwepo wa mwingine. Ukiatazama vizuri asili yao, bila kutaja kiasi cha pesa kilichowekwa kwa ajili ya kukamilisha kazi zao, vilabu hivi vinaweza kuwa na mapambano makali kuliko ilivyowahi kutokea kwenye miaka ya hivi karibuni.
Kuelekea mchezo wa huo dhidi ya United, tayari Guardiola ameshasema kwamba hana nia ya kuleta malumbano na hasimu wake: "Ni mchezo wa kirafiki. Tena wa kirafiki haswa." hata Mourinho mwenyewe anaonekana kutotaka kurudi katika zile zama za 'mind games'. Lakini pengine hii ni rahisi kusema kwasababu kwa sasa hakuna presha yoyote ile.
Baada ya miaka kadhaa ya mpito, sasa vilabu vya jiji la Manchester vinarudi, kwa maana ya ubora wa uwanjani na kwenye masuala ya usajili licha kwamba itachukua muda kidogo, lakini Guardiola na Mourinho watarajie kuwa 'centre of attention' na kuanzia mchezo wa leo mengi yataanza kuzungumzwa.
0 comments:
Post a Comment