Sunday, May 15, 2016

Real Madrid kwa mara nyingine tena wameshindwa kutwaa ndoo ya La Liga licha ya kupata ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wao wa jana dhidi ya Deportivo La Coruna.
Mabao yote mawili ya Real Madrid yalifungwa na mpachika mabao hodari wa timu hiyo Cristiano Ronaldo.
Mabao hayo ya Ronaldo yamemfanya aweke rekodi mpya ulimwenguni na kuwa  mchezaji wa kwanza kabisa duniani kufunga mabao zaidi ya 50 kwenye ngazi ya klabu kwa misimu sita mfululizo.
Mshambulizi huyo raia wa Ureno ameweza kufunga mabao 35 msimu huu La Liga.
Lakini kitu pekee kinachozidi kumpa wakati mgumu Ronaldo ni hali ya kuwa ameshinda La Liga mara moja tu tangu asajiliwe klabuni hapo mwaka 2009 huku akishinda Copa Del Rey mara mbili tu, bila kusahau ubingwa wa Klabu Bingwa barani Ulaya.

Hii ndiyo rekodi ya jumla ya magoli ya Ronaldo kwa misimu sita mfululizo:
2010/11 – magoli 53
2011/12 – magoli 60
2012/13 – magoli 55
2013/14 – magoli 51
2014/15 – magoli 61
2015/16 – magoli 50

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video