Jamie Vardy na Riyad Mahrez wamepewa heshima maalum kuelekea mchezo wa mwisho wa kumaliza msimu wa Ligi Kuu nchini England, baada ya kampuni ya Nike kuwatengenezea viatu maalum vya mipira vilivyobeba majina yao kwa muunganiko. Hali hiyo imekuja kutoka na uwezo na ushirikiano wao mkubwa waliouonesha kwenye ligi.
Washambulizi hao wawili kwa pamoja wamefanikiwa kuwa na muunganiko bora uliowaletea kwa pamoja mabao 41 na kuwapa ndoo ya EPL na kuwazidi Tottenham ambao walikuwa wakiwafukuzia kwa karibu bila ya kusahau Manchester City and Arsenal.
Unstoppable together. ⚽️👉— Jamie Vardy (@vardy7) May 13, 2016
🙏 @NikeUK for our Vahrez Hypervenom II iD. Get yours: https://t.co/v0mqEPkmM0 pic.twitter.com/QvxUv0nqSm
Kwa kutambua uwezo wao, wametoa viatu maalum kwa wawili hao vyenye jina la 'Vahrez'.
Viatu hivyo vyenye mchanganyiko wa rangi nyeusi, nyeuoe na bluu kwa mbali, vitavaliwa na wawili hao kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Chelsea katika dimba la Stamford, mchezo ambao utafunga rasmi pazia la EPL msimu wa 2015-16, huku wakipewa heshima ya Gwaride maalu maarufu kama 'Guard of Honour' na Chelsea.
Kwa upande wake, Vardy alisema: "Mchezo wa mwisho wa ligi unatarajiwa kuwa maalum kwetu, nafahamu fika maelewano mazuri niliyonayo na Riyad – Ni kitu ambacho najivunia sana na hivi viatu vinaashiria yote hayo."
Wakati huohuo Mahrez aliongeza: "Mimi na Jamie tumepitia safari ndefu sana mpaka kufika hapa– ninafarijika sana kuvaa viatu hivi ikiwa kama alama ya mafanikio yetu msimu huu."
0 comments:
Post a Comment