Thursday, April 14, 2016

MWISHONI wa wiki iliyopita beki  tegemeo wa Azam FC, Shomari Kapombe, alikimbizwa nchini Afrika Kusini ili kupata matibabu ya haraka baada ya kugundulika kuwa ana ugonjwa wa Pulmonary Embolism (donge la damu kuziba mishipa ya damu katika mapafu).

Ugonjwa huo utamlazimu beki huyo wa zamani wa Simba na AS Cannes ya Ufaransa, kukaa nje kwa miezi mitatu na maana yake hatacheza tena msimu huu.

Beki huyo kwa siku za karibuni amekuwa na kiwango kizuri kwani mpaka sasa ameshaifungia Azam FC mabao 11, nane kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), mawili Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) na moja amefunga ndani ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC) wakati timu hiyo ikiilaza Bidvest Wits mabao 3-0.

Kitendo cha kukosekana kwake tayari kocha wake, Stewart Hall, amelazimika kupangua mfumo wake wa 3-5-2 ili kuiwezesha timu hiyo kufanya vema kwenye michezo yake iliyosalia bila kuwa na Kapombe.

Kufuatia kukosekana kwa beki huyo, BINGWA limemtafuta daktari Nassoro Matuzya, ili kuzungumzia kiundani kuhusu ugonjwa huo unaomsumbua beki huyo ambaye pia ni tegemeo kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’.

 Pulmonary Embolism ni nini?

Ni tatizo la kukwama ghafla kwa mishipa ya damu inayoitwa ‘artery’ katika mapafu kutokana na kuganda kwa damu (kuvilia) mara nyingi damu iliyoganda ni chache na sio kama imekufa, lakini inaweza kuharibu mapafu, lakini pia kama mgando wa damu ni mkubwa inaweza kusababisha damu isitembee. Pia ugando huo unaweza ukawa ni ule ambao hauna uhai. Na hapo ndipo matibabu ya haraka yanafanyika ili kuokoa maisha ya mhusika.

 Dalili zake

Kuhema haraka haraka, maumivu makali ya kifua ambayo yanaongezeka wakati wa kukohoa au kuvuta hewa ndani au kupumua kwa nguvu.

Kukohoa makohozi ya pink au kama ute wa povu, lakini pia inaweza kuonyesha dalili nyingine kama mtu anaweza kuwa rahisi kukasirika, kutoka jasho kwa wingi na kuona kama kichwa ni chepesi au kupoteza fahamu na mapigo ya moyo kwenda kasi.

Sababu za ugonjwa huo

Ugonjwa huu unaweza kusababishwa na kitu chochote mfano kuumia kwa aina yoyote, kuwa na marathi yoyote yanayohusiana na damu kama Porphylia, Thalasaemia na Thrombosis ambayo ukiwa nayo unaweza kupata tatizo hilo la ‘Pulmonary Embolism’ au hata kugongana na mtu uwanjani.

Ugonjwa huu unaweza ukatokea kwenye mapafu, ubongo na hata ini ambapo sababu kuu ni kuingia kwa vipande vya damu kwenye mishipa inayosababishwa na kuvilia kwa damu.

Kinga za ugonjwa

Kinga kubwa ni kwa madaktari mbalimbali kuwa makini katika kipindi cha upasuaji ili kuzuia damu isigande hususani kwenye mishipa ya damu.

Kinga nyingine ni kufanya mazoezi mara kwa mara ili kutoruhusu damu kuganda na kurahisisha mzunguko wa damu kufanya kazi kwa haraka.

Kinga ya mwisho ni kujizuia kutumia vyakula vyenye mafuta zaidi ili kuepuka ugonjwa huu.

Takwimu za ugonjwa huo

Takwimu zinasema kuwa sio ugonjwa unaosumbua sana ndio maana hakuna takwimu za wagonjwa huo lakini inaweza ikawa tatizo kama itatokea kwenye moyo ndio inakuwa madhara zaidi.

“Hatuna takwimu, inaweza ikawa haijagundulika mapema, sio tatizo ambalo linasumbua sana, ikitokea kwenye moyo ndio utakuta moyo unasimama, kitakwimu hakuna ila inatokea mara chache ndio maana hatuna takwimu,” alisema Matuzya.

Matibabu yake

Matibabu ya ugonjwa huo mara nyingi ni upasuaji ili kuondoa mapande hayo ya damu au kama sio upasuaji basi mgonjwa atatumia dawa au sindano pindi mgonjwa atakapoanza matibabu.

“Sipaswi kusema ni aina gani ya dawa mgonjwa anapaswa kutumia au sindano gani ila jua matibabu yake ni dawa au sindano na kingine ni upasuaji ili kuondoa mapande hayo ya damu,” alisema.

Mgonjwa anatumia muda gani kupona

Ugonjwa huo unategemea maradhi yalivyoanza kugundulika na jinsi alivyoanza matibabu mfano kwa Kapombe amepewa mapumziko ya miezi miwili hadi mitatu ili kuweza kurejea katika hali yake ya kawaida.

“Inategemea na maradhi yalivyogundulika halafu matibabu mapema na ndio yanaweza kumnusuru mgonjwa,” alisema Matuzya.

Kapombe atarejea kama kawaida uwanjani?

Alipoulizwa kama Kapombe ataweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida Matuzya, alisema kuwa hakuna kitakachomzuia beki huyo wa timu ya Taifa kwa sababu tayari ameanza matibabu.

“Atarejea kama kawaida uwanjani hakuna kitakachomsumbua huu ni ugonjwa kama mwingine na kwa sababu ameshaanza matibabu basi atarejea bila shaka,” alisema.
Credit:Bingwa

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video