Hassan Isihaka (kulia) akiwa na Ibrahim Ajib wakishangilia moja ya mabao msimu huu.
Klabu ya Simba, imetangaza kumsimamisha beki wake Isihaka Hassan kwa mwezi mmoja.
Pamoja na kumsimamisha, imetangaza kumvua unahodha msaidizi pale atakaporejea kundini. Hii ni kutokana na madai ya kumjibu kwa lugha isiyo ya kiungwana Kocha wake, Jackson Mayanja alipotaka kumpanda acheze katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United.
Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati alipozungumzia suala la utovu wa nidhamu lililokuwa likimkabili Isihaka ambaye alisimamishwa kwa muda usiojulikana.
Uamuzi huo wa kumsimamisha ambao ni sehemu ya uamuzi wa kamati ya utendaji.
Siku Manara alipotangaza kumsimamisha Isihaka kwa muda usiojulikana, mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza aliandika mtandaoni kwamba mchezaji huyo alikuwa anaonewa na kuchafuliwa jina.
Lakini siku iliyofuata, isihaka alimuaibisha Kiiza kwa kuomba radhi kutokana na kosa la kuzungumza kwa lugha isiyo ya kiungwana mbele ya kocha wake na wachezaji wengine.
Uongozi wa Simba ukampa onyo pia na kumtaka azikanushe habari hizo ambazo zilionekana zinalenga kutetea watovu wa nidhamu.
Credit:Salehjembe
0 comments:
Post a Comment