Wednesday, March 16, 2016

Azam FC imeutumia vyema mchezo wake wa kiporo kwa kuichapa Stand United ya Shinyanga kwa bao 1-0 kwenye mchezo pekee wa ligi uliosukumwa kwenye uwanjawa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Bao pekee lililoipa Azam pointi tatu limefungwa na Shomari Kapombe dakika ya 62 akiunganisha krosi iliyopigwa na John Bocco ‘Adebayor’ aliyeingia kwenye mchezo huo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Allan Wanga.
  • Stand United hawajashinda mechi yeyote katika mechi zao nne zilizopita kwenye ligi, wamepoteza mchezo wa nne leo dhidi ya Azam FC; Tanzania Prisons 1-0 Stand United, Mbeya City 2-0 Stand United, Majimaji 1-0 Stand United na leo tena Stand wamepoteza mchezo wao wan ne mfululizo Azam FC 1-0 Stand United.
  • Licha ya Azam kushinda na Stand kupoteza, bado timu hizo zimeendelea kusalia kwenye nafasi zao zilezile. Azam nafasi ya tatu ikiwa na pointi 50 ikiwa imecheza michezo 21 sawa na Yanga lakini zikiofautiana magoli ya kufunga na kufungwa. Yanga iko nafasi ya pili Azam inasalia nafasi ya tatu. Stand yenyewe inabaki katika nafasi yake ya saba ikiwa na pointi 30 nyuma ya Mwadui yenye pointi 34.
  • Shomari Kapombe amefunga goli lake la saba (kwa mujibu wa takwimu za TFF) akiwa ndiye beki mwenye magoli mengi zaidi. Pia ni goli lake la pili kwenye mechi mbili mfululizo baada ya kufunga goli moja kwenye mchezo wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini.
  • Mechi zijazo zinazozihusu Stand na Azam, Stand watakuwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Kambarage Stadium kuwakaribisha Ndanda FC wakati Azam yenyewe itasafiri kwenda Mwanza kuikabili Toto Africans kwenye uwanja wa CCM Kirumba.
  • Stand wamepoteza jumla ya pointi 12 kwenye mechi nne, endapo wangeshinda mechi zote wangekuwa na pointi 42 ponti nyingi zaidi ya Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya nne ikiwa na pointi 39.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video