Saturday, March 12, 2016

Rafa Benitez jana amekabidhiwa rasmi mikoba ya kukinoa kikosi cha Newcastle United ambacho kiko taaban kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.
Baada ya tu ya kutabgazwa rasmi kuwa kocha, alianza mara moja kukinoa kikosi hicho jana hiyo hiyo.
Kabla ya kutua Newcastle, Benitez alikuwa meneja wa Real Madrid ya nchini Uhispania ambako alitimuliwa kutokna na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo hasa kile kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa FC Barcelona.
Benitez amechukua mikoba ya Steve McClaren ambaye ametimuliwa Newcastle kutokana na mwenendo mbovu wa klabu hiyo.
Baada ya kukabidhiwa mikoba hii, hizi ndizo mechi ambazo kama Benitez atatoboa na kuibakisha Newacstle EPL, basi jina lake halitasahaulika klabuni hapo.

Mechi kumi za kuamua Newcastle ibaki au iondoke EPL
March 14 Leicester City (A)
March 20 Sunderland (H)
April 2 Norwich City (A)
April 9 Southampton (A)
April 16 Swansea City (H)
April 23 Liverpool (A)
April 30 Crystal Palace (H)
May 7 Aston Villa (A)
May 15 Tottenham (H)

TBC- Manchester City (H)

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video