Saturday, March 12, 2016

Bado Simba ina nafasi kubwa ya kubeba ubingwa wa Tanzania Bara na kocha wake, Mganda Jackson Mayanja anashangazwa na wanaoibeza.
Mayanja amesema mbio za ubingwa zitaendelea kubaki kwa timu tatu ambazo ni Simba, Yanga na Azam FC lakini si sawa kuona kati ya hizo tatu, moja ina nafasi zaidi.
“Nafasi tunayo, tena kubwa tu hata kama wenzetu wana michezo mkononi. Huwezi kujua wakicheza itakuwaje maana bado hawajapata matokeo,” alisema.
Mayanja alisema kazi kubwa wanayofanya kazi katika kikosi chao ni kuhakikisha wanashinda mechi zao tu.
“Sisi tunahitaji pointi tatu, wenzetu watafanyaje inakuwa ni ya kwao,” alisisitiza.
Simba ipo kileleni  mwa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 51 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 50 na Azam FC yenye pointi 47. 
Lakini Yanga ina michezo miwili mkononi wakati Azam FC ina michezo miwili ya viporo.
Credit:Salehjembe

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video