
Bado hakuna uhakika kama mshambuliaji hatari wa Yanga, Amissi Tambwe ataivaa APR ya Rwanda kwenye Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, leo.
Hofu ya Tambwe imeanza baada ya kusema anajisikia vibaya lakini bado Yanga wanavuta subira.
Yanga ipo mjini Kigali kuivaa APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Katika mazoezi ya mwisho ya Yanga, Tambwe alianza kufanya mazoezi peke yake kwenye Uwanja wa Katika mazoezi yake kwenye Uwanja wa Amahoro enero la Remara jijini Kigali.
Lakini baadaye akaungana na wenzake na kuendelea kufanya nao mazoezi mepesi.
Kocha Msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi amesema wataendelea kusikilizia ili kujua hali yake.
“Kweli anaumwa, lakini hatujajua kama atakuwa katika kiwango kipi. Ni suala la kusubiri na kesho tutakuwa na jibu,” alisema.
Chanzo:Salehjembe
0 comments:
Post a Comment