Habari zilizothibitishwa na madaktari nchini Iceland zinasema, kipa wa zamani wa klabu ya Simba SC ya Tanzania, Abel Dhaira anasumbuliwa na kansa ya tumbo (Abnominal Cancer)
Kipa huyo ambaye alikuwa anachezea klabu ya IBV Vestmannaeyjar nchini humo, awali kwa nyakati tofauti alikuwa akilalamika kwamba anasumbuliwa na vidonda vya tumbo (ulcers), typhoid pamoja na maumivu ya kawaida ya tumbo (abnominal pain) kwa kipindi kirefu.
Mganda huyo ambaye pia ameshachezea klabu za URA na Express zote za Uganda, alidaka mechi ya mwisho na IBV mwezi October 2015, na aliomba kupumzika baada ya kuona anajisikia vibaya kiafya.
Aliamua kurudi nchini Uganda kutembelea familia yake ambapo afya yake ilianza kuzorota January 2016 na kukimbizwa hospitali ya Nsambya jijini Kampala ambapo amelazwa kwa wiki 6 sasa.
PICHANI JUU ni Dhaira akiwa majukumuni kipindi chake akichezea Uganda Cranes, na Simba SC. Picha nyingine ni akiwa hospitalini na kocha mkuu wa IBV, Bjarni Jóhannsson.
0 comments:
Post a Comment