Wednesday, March 16, 2016

Manchester City itakuwa bila ya nahodha wake Vincent Kompany kuelekea katika mchezo dhidi ya Manchester United mwishoni mwa wiki hii baada ya kutonesha jeraha lake la nyama za nyuma ya ugoko.
Kompany amecheza michezo 13 tu ya Ligi Kuu England msimu huu kutokana na kuwa nje kwa majeraha, na kurudi katika mchezo wa jana kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Dynamo Kiev.
Hata hivyo, hakuweza kumaliza mchezo huo kutokana na kuumia katika dakika ya saba tu ya mchezo na kutolewa nje, na hivyo kocha wake Manuel Pellegrini kuthibitisha kukaa nje kwa mwezi mmoja.
"Vincent, kwa bahati mbaya amepata maumivu ya misuli ya nyuma ya nyama za mguu kama yaliyokuwa yakimsumbua awali," alisema.
Tangu ajiunge na vigogo hao wa jiji la Manchester mwaka 2008, Kompany amekumbana na majeraha ya aina hiyo takriban mara 14.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video