Thursday, March 17, 2016

Arsenal waliingia katika mchezo wa jana wakiwa ama hawana nafasi kabisa au wana nafasi finyu ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hapa chini ni baadhi ya mambo ambayo yameonekana katika mchezo wa jana;

Vikosi vya timu zote mbili 
Kwa kuanzia na Barcelona ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo, kulikuwa na mabadiliko ya mtu mmoja tu ukilinganisha na kikosi kilichoanza dhidi ya Arsenal katika raundi ya kwanza, Jeremy Mathieu alianza akichukua nafasi ya Gerald Pique aliyekuwa na kadi mbili za njano. Utatu mtakatifu unaoundwa na Luis Suarez, Neymar na Lionel Messi kama ilivyoada ilikuwa ni kupeleka kilio kwa washika bunduki wa London.

Kwa upande mwingine, Arsenal ambao alikuwa wageni katika mchezo huo, walifanya mabadiliko ya wachezaji sita katika kikosi chao ukilunganisha na kile kilichoanza wiki mbili zilizopita.
Lakini 'talking point' hapa ni Alex Iwobi  na Flamini ambaye wamemtunga jina la  “master of ceremony” wa mchezo wa kwanza baada ya kunogesha ushindi wa Barcelona kutokana na kumfanyia madhambi ndani ya eneo la 18 punde tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Francis Coquelin.
Iwobi ambaye ni kinda wa Kinigeria alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu bora ulimwenguni. Alikuwa akipambana kwenye eneo la kiungo na wachezaji kama Iniesta, Rakitic na Busquests ambapo katika hali ya ni jambo lisiloweza kuelezeka kwamba inawezekanaje Iwobi kupambana na nyota hao kutokana na namna walivyo na uwezo mkubwa.

Mbinu za kiufundi
Wakicheza kwa kujiamini na kutumia  mfumo uliozoeleka tangu enzi za kocha wao wa zamani Pep Guardiola, Barcelona walikuwa hawana presha kubwa kutokana na kuwa na hazina ya mabao mawili waliyopata katika dimba la Emirates wiki mbili zilizopita. 
Arsenal wana tabia ya kucheza mpira wa aina moja na Barcelona lakini uwezo wao mdogo wa mchezaji mmoja mmoja huku wakati huo huo wakidaiwa magoli mawili kuliwafanya wapoteze kujiamini na kukosa mwamko wa kuitoa Barca. 
Wakati Barcelona wana wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote, wao Arsenal wachezaji wao wengi wao ni 'tia maji tia maji'
Arsene Wenger alisema kuwa wao walienda pale kwa dhumuni la kushambulia tu ili kufanya yasiyowezekana kuwezekana. Kwa kufanya hivyo akaamua kuwaanzisha wachezaji wenye kasi kama vile Danny Welbeck, Alex Iwobi na El Neny ili kufanya mashambulizi ya kushtukiza japo hawakufanikiwa kutokana na watatu hao kukosa umakini golini. 
Kuanzia katika eneo la kiungo mpaka safu kali kabisa ya ushambuliaji, Barcelona ina wachezaji ambao muda wowote wanaweza kubadilisha matokeo ya mchezo, kwa mafano ' Katika mchezo wa jana, makosa madogo yaliyofanywa na mabeki wa Arsenal yalitosha kumpa Messi nafasi ya kuwaangamiza Arsenal.

Arsenal kwa namna nyingine imekuwa ni timu inayomtegemea maajabu ya Ozil na akibanwa tu basi kila kitu kinashindikana. 
Mchezaji bora wa Arsenal msimu uliopita Alexis Sanchez amekuwa hayuko katika kiwango bora msimu huu na katika mchezo wa jana amefanya 'slides' na 'slips' nyingi kuliko mashuti yaliyolenga langoni.
Ozil naye ni mchezaji ambaye amekuwa aking'ara pale timu inapokuwa iki-possess mpira na ndipo ambapo mara nyingi madhara yake huonekana, lakini pale timu inapokuwa imeelewa kamwe hutamwona kama Ozil ni mchezaji mzuri.

Kukosekana kwa 'consistency' katika timu.
Tatizo kubwa la Arsenal kwa miaka mingi limekuwa ni kukosekana kwa 'consistency' hasa wanapotakiwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya timu. Pengine hali hii inatokana na uwepo wa wachezaji kutoka katika akademi ya klabu hiyo ambao mara nyingi wanaamini katika kupiga pasi nyingi ili wapandishwe timu ya wakubwa. 
Wanakosa matamanio ya kuwa mabingwa tofauti na inavyoonekana kwa wachezaji wa timu nyingine.
Mtazamo wa wachezaji wa Arsenal lazima ubadilike ili waweze kuendana na ushindani uliopo sasa. Hiyo ndiyo itawarudisha katika enzi za 'invisibles'.
Suala la mwisho ni kwamba, katika mchezo wa jana Barcelona waliitawala Arsenal kwenye kila idara, lakini vile vile Arsene Wenger bado ni kocha mzuri ila kuna mambo anayotakiwa kukubali kubadilika, hasa katika suala la ununuzi wa wachezaji wenye majina makubwa na wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo uwanjani pindi timu inapohitaji kufanya hivyo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video