
Mbio za kuepuka kushuka daraja zimezidi kunoga baada ya timu ya Majimaji kuibuka na ushindi dhidi ya Mbeya City na kuongeza matumaini ya kubaki.
Majimaji imeinyuka Mbeya City kwa mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa hii leo kwenye Uwanja wa Majimaji mjoni Songea.
Katika mchezo huo, Majimaji ambayo ilikuwa na kumbukumbu za kuchukua alama tatu katika mchezo uliopita dhidi ilionekana kupania mchezo huo tangu filimbi ya kuanza ilipopulizwa.
Wenyeji walijipatia mabao yao kupitia kwa Danny Mrwanda ambaye aliyefunga bao la kwanza na mengine yakifungwa na Masel. Kwa upande wa Mbeya City, bao lao la kufutia machozi liliwekwa kimiani na Juma Abdallah.
Kwa matokeo hayo, Majimaji wamefikisha pointi 27 wakati Mbeya City imebakia na pointi 24 katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na Simba yenye pointi 57.
Katika mchezo mwingine, Stand United ilishindwa kutamba katika uwanja wake wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya mabao 1-1 na Ndanda.
0 comments:
Post a Comment