
Wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wamesonga mbele kwenye michuano hiyo kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na APR kwenye mchezo uliovurumishwa kwenye dimba la Taifa jijini Dar es salaam.
Yanga ambao ni mabingwa wa Tanzania msimu uliopita, inafanikiwa kusonga mbele kufuatia ushindi wa mabao 2-1 walioupata wikiendi iliyopita nchini Rwanda na kuifanya itinge hatua inayofuata kwa jumla ya mabao 3-2.
APR ndio waliokuwa wa kwanza kuandika bao kwenye dakika ya tatu ya mchezo kupitia kwa Fiston Nkinzi ngabo baada ya kutumia vizuri makosa ya walinzi wa Yanga na kumchungulia mlinda mlango Ally Mustapha kabla ya kuachia mkwaju uliotinga moja kwa moja kimiani.
Baada ya kuingia kwa bao hilo, Yanga walionekana kuamka na kuanza kufanya mashambulizi na iliwachukua dakika 25 kupata bao la kusawazisha lililowekwa kambani na mshambuliaji wake hatari, Donald Ngoma lililotokana na uwezo wake binafsi.
Iliwachukua takribani dakika 18 za kipindi cha kwanza APR kuliegemea lango la Yanga na kuonyesha uhai wa kupata bao la mapema.
Kwenye mchezo huo Yanga ilionekana kupoteza nafasi za wazi hasa kxwenye dakika ya 10 baada ya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuandika bao na kwenye dakika ya 22 kiungo mshambuliaji wa Yanga, Thabani Kamusoko alikaribia kuipatia timu yake bao baada ya kuunganisha pasi ya Haruna Niyonzima.
Winga wa kushoto wa APR alipiga kona iliyozua kizaazaa langoni mwa Yanga ikiwa kwenye dakika ya 18 ya mchezo ikiwa ni dakika nne baada ya Ally Mustapha kudaka mpira wa adhabu ndogo.
Kama haitoshi wanajangwani hao walikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuandika bao la pili ikiwa ni baada ya Deus Kaseke kupiga krosi kwenye dakika ya 34 hata hivyo haikuzaa matunda ikiwa ni dakika mbili baada ya Yanga kukosa bao kupitia mpira wa adhabu ndogo.
Mlinda mlango wa Yanga, Ally Mustapha aliiokoa timu yake baada ya kupigwa mpira kutokea kwenye robo tatu ya mwisho ya eneo lao la hatari kwenye dakika ya 59 ya mchezo huo uliookekana kuwa na mabadiliko makubwa kwa timu zote kushambuliana hapa na pale.
Mlinzi wa kati wa Yanga, Vincent Boussou alizidi kuimarisha safu yake ya ulinzi baada ya kuondosha mpira wa hatari langoni make. Latlkini Geoffrey Mwashiuya alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kuiandikia Yanga bao la kuongoza baada ya shuti lake kutoka sentimita chache langoni mwa APR kwenye dakika ya 88 ya mchezo.
Credit:Soka 360.
0 comments:
Post a Comment