Wednesday, March 2, 2016

Jackson Mayanja-Kocha wa Simba SC.
Baada ya mlinzi na nahodha msaidizi wa Simba Hassan Isihaka jana kuomba radhi mashabiki pamoja na kocha wa Simba kwa wakati huu Jackson Mayanja kwa kile ambacho kilitokea na kupelekea nyota huyo kusimamishwa kwa madai ya kumtolea maneno makali kocha huyo, Mayanja ameibuka na kutoa kauli yake.
“Mimi sina tatizo kwa sababu nasimamia maadili ya mpira. Sina shida kabisa na Isihaka kama mchezaji lakini tatizo ni maadili ya kazi yetu kwasababu mimi nasimamia maadili ya mpira” anasema kocha huyo ambaye anadai kusimamia zaidi maadili ya soka kuliko kuangalia jina la mchezaji.
“Sitaki kuongea sana kuhusu Isihaka kwasababu ni mchezaji wa Simba kama walivyo wengine lakini kitu nachojua mimi, hakuna mchezi ambaye yuko juu kuliko klabu duniani kote”.
“Ndiyomaana hata ukiangalia Ulaya Cristiano Ronaldo alikuwa anapendwa na mashabiki wa Manchester United lakini aliuzwa na timu imebaki na hata Simba na Yanga wachezaji wengi wameshapita lakini vilabu bado vimebaki”.
Inadaiwa Isihaka alimtolea kocha wake maneno yasiyo ya heshima baada ya Mayanja kutompanga kwenye mechi ya ligi kuu dhidi ya Yanga kisha kumpanga kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United.
Uongozi wa Wekundu wa Msimbazi ulichukua uamuzi wa kumsimamisha Isihaka kwa muda usiojulikana.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video