Sunday, March 20, 2016

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho Azam Fc, imetinga raundi ya pili ya kombe la Shirikisho CAF baada ya kuifunga Bidvest mabao 4-3, mchezo uliopigwa kunako dimba la Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Azam ndiyo walioanza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua takriban dakika ya 23 pale Ramadhani Singano 'Messi' alipokimbia na mpira kwa kasi katika winga ya kulia na kuaachia krosi iliyotua kichwani mwa Kipre Tchetche na kuifungia Azam bao la kwanza. 
Azama walizidi kulisakama lango la Bidvest huku Kipre Tchetche ambaye alikuwa mwiba kwa mabeki wa Bidvest, alipanda kwa kasi na kupiga krosi ambayo ilimaliziwa nyavuni na John Bocco. 
Huku na kule wakati Azam wakiwa hawajamaliza kusherehekea bao hilo, mshambuliaji aliyeingia kuchukua nafasi ya Pule, Jabulani Shongwe aliifungia Bidvest bao la kwanza katika dakika ya 43 baada ya uzembe uliofanywa na mabeki wa Azam.
Alikuwa ni Kipre Tchetche kwa mara ya pili alipofanikiwa kutegua mtego wa kuotea uliowekwa na walinzi wa Bidvest kisha akampiga chenga kipa Jethren Barr na kufunga bao la tatu kwenye dakika ya 54 kabla Koiekantse Mosiatlhaga kuwarudisha kati Azam baada ya kuwafungia bao la pili 'wasauzi' hao. 
Tchetche alifunga bao lake la tatu (hat-trick)na la nne kwa Azam katika dakika 87 baada ya kuwatoka walinzi wa Bidvest na kuachia shuti kali. Wakati mpira watazamaji wakianza kuinuka vitini, Henrico Botes aliipatia Bidvest bao tatu.
Azam imesonga mbele kwa jumla ya mabao 7-3 na sasa itapambana na Esperance ya Tunisia ambayo imeitoa Renaissance kwa jumla ya mabao 7-0

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video