
Arda Turan ametanabaisha kuwa, kuchezea klabu kama Barcelona ni zawadi kubwa iliyotokana na uwezo wake uwanjani na kufiti na staili ya uchezaji wa timu hiyo, ama vinginevyo angekuwa akicheza klabu kama Arsenal.
Mturuki huyo ambaye hakupata nafasi ya moja kwa moja kucheza Barcelona, wakati aliposajiliwa kutokana na klabu hiyo kutumikia kifungo cha kutosajili mchezaji yeyote, amefanikiwa kuingia katika kikosi cha kwanza mapema mwaka huu baada ya kiwango bora alichoonesha klabuni hapo.
Arda amesisitza kwamba, wachezaji wote wenye viwango bora huishia kwenye klabu kama Barcelona na kupata mafanikio hapo, na wale wenye viwango vya kawaida huishia kwenye klabu yenye maskani yake kaskazini mwa jiji la London (akimaanisha Arsenal).
"Nilihisi kwamba ningesajiliwa na Barcelona. Lazima niwe mkweli, mara zote nilikuwa nikifikiri hivyo, 'kama nitacheza vizuri, basi nitasajiliwa na Barcelona, kwa sababu staili yangu inafiti kwenye timu hii," alisema Arda.
"'Kama nitacheza vizuri, nitaenda Arsenal, lakini endapo ningekuwa na kiwango cha kawaida"
"Kwa sababu staili ya uchezaji wangu, kuwa mrahisi kwenye mpira, kupiga pasi fupi fupi, kutumia nguvu inapobidi, lakini zaidi nikicheza soka lenye ubora wa hali ya juu, nilifahamu fika kwamba ningejiunga moja kwa moja na Barcelona."
0 comments:
Post a Comment