Saturday, March 12, 2016

Ibrahimu Ajibu.
STRAIKA wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amewataja Ibrahimu Ajibu na Joseph Kimwaga kwamba wakiongeza juhudi na kutambua kwamba soka ni kazi yao basi wanaweza kuwa mfano wa kuigwa ligi kuu.
“Kwa nafasi niliyokuwa nacheza Simba mpaka sasa hakuna ambaye amefikia uwezo wangu ila Ajibu, Kimwaga wanaweza kunifikia na kunizidi lakini lazima waelekeze akili zao katika kujituma kwa bidii na kupambana,” alisema.
Nyota huyo alisema mchezaji mwenye kipaji anaonekana hata kama ataonyesha udhaifu kwenye mechi lakini kunakuwa na vitu anavyokuwa anavifanya vinavyoonyesha kipaji chake, jambo la msingi ni kuwaongezea nguvu na kuwaelekeza kujua wao ni kina nani kwenye ulimwengu wa soka.
“Ni wachezaji wazuri siku wakiamua Tanzania itakuwa imepata vifaa siyo Simba pekee natazama jicho la mbali hadi kwenye Taifa Stars ila sharti ni wao wenyewe wawe tayari kujituma na kuipenda kazi yao,” alisema.
Akiizungumzia Simba alisema kwamba wakitumia nguvu nyingi katika kupambana bila kujali kejeli zinazoelekezwa kwao watakuwa na nafasi kubwa ya ubingwa kwani hadi sasa haijulikani unaelekea Yanga ama Azam.
“Silaha kubwa ni adui yako anapoongea wewe unatumia maneno yake kumwangamiza kwa vitendo, waangalie nafasi na siyo kujibizana kwa maneno, hilo litaweza kurejesha heshima yao,” alisema.
Credit:Mwanaspoti.


0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video