Uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga umegeuka shubiri kwa vigogo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kushuhudia leo AZAM FC ikifungwa bao 1-0 na Coastal Union, hiki kikiwa ni kipigo cha kwanza cha Azam tangu msimu uanze.
Beki wa kulia wa Coastal Union Miraj Adam ndiyo alikuwa muuaji wa Azam FC aliyetikisa nyavu dakika ya 67.
Adam pia aliingia katika rekodi dhidi ya Yanga baada ya kufunga goli katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga SC na kuvunjwa mwiko wa kutofungwa msimu huu
Leo pia alifunga kwa shuti la mpira wa adhabu baada ya kuanzishiwa mpira na mlinzi mwenzake wa pembeni Adeyum Saleh Ahmed.
Kwa matokeo haoy Coastal Union imefikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi 19 na kupanda hadi nafasi ya 13, kutoka ya 16 ilipokuwa inashikilia mkia, wakati Azam FC inabaki na pointi zake 42 za mechi 17, nyuma ya Yanga SC yenye pointi 43 za mechi 18 na Simba SC pointi 45 za mechi 19.
0 comments:
Post a Comment