Sunday, February 14, 2016

Arsenal forward Theo Walcott (centre) celebrates after scoring the equalising goal against Leicester at the Emirates Stadium on Sunday
Arsenal wamezidi kuwapa matumaini ya ubingwa mashabiki wao baada ya kuwafunga kwa shida vinara wa ligi hiyo Leicester City kwa mabao 2-1.
Leicester walikuwa wa kwanza kupata bao kwa mkwaju wa Penati uliofungwa na kinara wa upachikaji mabao EPL Jamie Vardy baada ya kufanyiwa madhambi na beki wa Arsenal Nacho Monreal.
Arsenal walijitutumua na kufanikiwa kusawazisha bao lao kupitia kwa Theo Walcott ambaye alitokea bechi mnamo dakika ya 71 kufuatia kuunganisha mpira wa kichwa uliopigwa na Olivier Giroud.
Danny Welbeck aliyekuwa nje kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha, ambaye pia pia aliingia kutokea bechi, aliifungia Arsenal bao la ushindi mnamo dakika ya tisini na kupunguza pengo dhidi ya wapinzani wao na kufikia pointi 2.
Arsena kwa sasa wapo nafasi ya pili wakiwa na 51 waakiwa nyuma ya Leicester wenye pointi 53.
Leicester walipata pigo baada ya beki wao wa kulia  Danny Simpson kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya 54 baada ya kumchezea madhambi Olivier Giroud.

Video ya magoli hii hapa

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video