Thursday, October 22, 2015

Polisi nchini Hispania wanafanya uchunguzi juu ya madai ya mwamuzi msaidizi ambaye inasemekana anapewa msukumo ili aipendelee Real Madrid katika mchezo wa El-Clasico dhidi ya Barcelona utakaopigwa Novemba 21 mwaka huu.
Kituo cha radio cha Cadena COPE kimevujisha nyaraka ambazo zimewasilishwa polisi na Jacinto Vicente Hernandez, ambaye ni mwanasheria aliyebobea katika masuala ya michezo.
Nyaraka hiyo yenye kurasa sita inaelezea kwa kirefu namna ambavyo afisa huyo, ambaye amekataa kutajwa jina kwa sababu za kiusalama, alipoambiwa kufanya mawasiliano ambayo yangewanufaisha Madrid katika pambano hilo la kukata na shoka.
Inapendekeza kwamba Kamati ya Waamuzi imependekeza kwamba mwamuzi huyo msaidizi kutoa maamuzi kwa sababu katika mchezo uliopigwa mapema msimu huu baadhi ya maamuzi yalikuwa yamejaa upendeleo kutoka kwa mwamuzi mwingine, hali iliyosababisha utata
“Mtu mmoja anijulishwa kuhusu mwamuzi ambaye alikuwa na matatizo na ambaye alitaka kuongea na mimi,” Vicente aliiambia SPORT baada ya kielelezo hicho kuvuja.
“Unaweza kulifanyia kazi hilo, hatoki Barcelona [kwa sababu kama ni hivyo asingeweza kuruhusiwa kuwa mwamuzi wa mchezo huo wa El-Clasico], lakini nilikuwa pale jijini kwa sababu maalum na tuliahidiana kukutana pale.
“Alieleza kila kitu kilichotokea na kusema alitaka kwenda kadharani kuzungumza juu ya presha anayopewa kwa sababu ndio sababu pekee ya kusafisha taswira ya soka la Hispania.”
Vicente anasema kuwa afisa huyo mwanzoni alitaka ushauri wa jinsi gani kuweka hadharani taarifa hizi, lakini alimshauri katika kesi hiyo isingekuwa jambo jema kuipeleka polisi.
Waamuzi wa mchezo wa Clasico bado hawajatajwa rasmi, na hawatatajwa mpaka wiki moja kabla ya mchezo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video