Ingawa suala limekuwa likienda kwa siri kubwa lakini ukweli ni kwamba Kocha
Dylan Kerr wa Simba ameishaeleza kutoridhishwa na kiwango cha Elius Maguri na
yuko tayari aachwe.
Habari za ndani kutoka ndani
ya Simba zimeeleza kocha huyo Mwingereza ameonyesha kutovutiwa na kiwango cha
Maguri, hivyo ameuambia uongozi unaweza kumuonyesha mlango wa kutokea.
"Ni kweli, kocha ndiye amesema kwamba haridhishwi na Maguri. Amefanya naye
kazi kwa zaidi ya mwezi sasa na anaona hafurahishwi naye.
"Kuhusiana na kumuacha kwenye kikosi ilikuwa ni siku ya Simba Day, lakini
unaona Maguri kwa nini hakutambulishwa. Ilitakiwa atambulishwe kama wachezaji
wengine, lakini akatolewa kabisa.
"Hapo utapata jibu
kwamba Maguri hana chake Simba ingawa inaonekana anakosekana wa kumueleza
ukweli," kilieleza chanzo.
Lakini jana mchana, Rais wa
Simba, Evans Aveva amesema suala hilo limerudishwa kwenye kamati ya usajili.
"Kocha ndiye alitaka
Maguri aondolewe kwenye kikosi siku ya Simba Day. Kumekuwa na malalamiko kutoka
kwa wadau kwamba tunawaingilia makocha, hasa klabu hizi kubwa za Simba na
Yanga.
"Sisi hatukutaka hilo
litokee, tukampisha kocha afanye kazi yake," alisema Aveva.
"Lakini suala la Maguri
liko kwenye kamati ya usajili, mnajua huyo ni mchezaji wetu kabisa,"
alisema Aveva.
Via Salehehjembe


0 comments:
Post a Comment