Hatimaye ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu mkoani Mbeya na maeneo mengine imewadia!
Leo Saa 10:00 jioni, mabingwa wa kandanda Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans wanacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Wenyeji, Mbeya City FC katika uwanja wa Sokoine.
Afisa habari wa Mbeya City, Dismas Ten amewasiliana na MPENJA SPORTS asubuhi hii akitaja maeneo ambayo tiketi zinapatikana.
Kama uko hapo Green City, nenda Kabwe, Soweto, Stand Kuu au Uwanja wa Sokoni ukachukue kibali hicho cha kuwaona wanaume wakitifuana.
Pia amethibisha kwamba kikosi chao kipo imara kuwakabili Yanga na maandizi yote, kimsingi, yamekamilika.
0 comments:
Post a Comment