Mabingwa wa soka Tanzania bara, Dar Young Africans
wanatarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Mbeya City FC katika uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya.
Mechi hiyo ya kukata na shoka itapigwa Jumapili ya Agosti 16
mwaka huu.
kikosi cha Yanga chini ya kocha Hans van der Pluijm
kimejichimbia mjini Tukuyu jijini humo, wakati wagonga nyundo wanaonolewa na Juma
Mwambusi wakiendelea kujifua dimba la Sokoine.
Mwishoni mwa Juma lililopita, Yanga iliichapa 4-1 Komondo FC
katika mechi ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa CCM Vwawa Mbozi.
Magoli ya Yanga yalitiwa nyavuni na Geofrey Mwashiuya
(Mawili), Amissi Tambwe na Simon Msuva.


0 comments:
Post a Comment