Kipa ambaye anatakiwa kwa hamu kubwa na Real Madrid bado ataendelea kukaa benchi kwenye mechi ijayo dhidi ya Aston Villa kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa ufunguzi.
Licha ya De Gea kusema kwamba yupo tayari kucheza kwa sasa, lakini kocha wake, Louis Van Gaal amesema kwamba hatacheza kwenye mechi ijayo.
De Gea atakosa hiyo safari kwasababu bado yupo kwenye hali ile ile iliyosababisha kukosa namba mechi ya kwanza ambayo ni kutokuwa sawa kisaikolojia.
De Gea anahusishwa sana na kuhama klabu ya Manchester United na Kwasababu kipindi cha usajili bado kipo, basi kipa huyo yupo kwenye tatizo hilo.


0 comments:
Post a Comment