Saturday, July 18, 2015

Leo saa 10 jioni katika uwanja wa Taifa kutakuwa na mchezo mkali utakaozikutanisha Yanga ya Tanzania dhidi ya Gor Mahia ya Kenya.Mpambano huu wa kundi A utakaoshuhudiwa na mgeni rasmi Ndg. John Pombe Magufuli umekuwa na vivutio vya aina yake.Kila upande ukijinasibu kuibuka na ushindi kwa kuamini uimara wa timu yake, ukiachana na upinzani wa maneno baina ya mashabiki wa pande mbili unaoendelea,kubwa zaidi ni ubora wa vikosi vyote viwili vinavyotoa taswira yenye hadhi ya fainali kwa michuano hii.
UBABE KATIKA LIGI ZAO.
Klabu ya Yanga ilionesha kiwango kizuri sana katika michuano yote iliyoshiriki kwa msimu 2014-2015 ikifanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara,safu ya ushambuliaji ndio ilikuwa tishio zaidi kwa kupachika goli 52 katika mechi 26 wastani wa goli 2 kwa kila mchezo,hivyo hivyo kwa Gor Mahia hadi hivi sasa katika ligi ya kwao ipo kileleni kwa tofauti ya alama 14 haijafungwa mchezo hata mmoja na ina wastani wa kufunga magoli 2 kwa kila mchezo.
WOTE MABINGWA MARA 5 WA KAGAME.
Yanga bingwa wa KAGAME mara 5, kwa mwaka 1975,1993,1999,2011 na 2012.
Hivyo hivyo kwa Gor Mahia nao ni mabingwa mara 5,kwa mwaka 1976,1977,1980,1981 na 1985.
Timu zote zipo mawindoni kusaka ubingwa wa 6 kuifikia rekodi ya Simba SC.
USHABIKI DAMU.
Yanga ndio klabu yenye mashabiki wengi zaidi ukifananisha na vilabu vyote vya ukanda huu wa CECAFA katika list hiyo ya 3 bora huwezi kuiacha Gor Mahia,sifa kubwa ya mashabiki wa vilabu hivi ni uzalendo haswaa kwa vilabu vyao.Jana mchana mamia ya mashabiki wa Gor Mahia walifanikiwa kuvuka boda ya Namanga kuingia nchini Tanzania,upinzani wa mashabiki umenogeshwa zaidi baada ya mashabiki wa Simba kuvamia sherehe kwa kuungana na mashabiki wa Gor Mahia kuinanga Yanga.
FALSAFA YA MAKOCHA.
Hans Van Pluijm huamini katika soka la kushambulia kama njia sahihi ya kujilinda na kupata ushindi pia hivyo hivyo kwa Frank Nuttal kocha wa Gor Mahia,hivyo leo ni mchakamchaka dakika zote 90.
Wachezaji hatari zaidi wa kutazamwa.(Yanga)
Donald Ngoma, Niyonzima, Msuva, Kaseke, Canavaro na Amis Tambwe.
Wachezaji wa kutazamwa (Gor Mahia)
Michael Olunga, Meddie Kagere, Boniface Olouch, George Odhiambo na Godfrey Walusimbi.
Kivutioa kingine pale raia wa Liberia watakapokuwa wanatoana jasho mshambuliaji wa Yanga Kpah Sean Sherman dhidi ya beki wa Gor Mahia Glay au Haruna Niyonzima dhidi ya Wanyarwanda wenzie Medie Kagere na Sibomana.
Hii ni fainali kabla hata fainali haijafikia ni fainali katika hatua ya Makundi, Yanga tunatamba kwa kuwa na timu nzuri Gor Mahia hawapo nyuma,hakuna asiyefahamu timu za Kenya zinapokutana na za Tanzania nini hutokea.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video