Saturday, July 18, 2015

Hatimaye nahodha wa zamani wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya England, Steven Gerrard ameanza vyema kuichezea timu mpya inayoshiriki Major League Soccer ya nchini Marekani, LA Galaxy.
Katika mechi ambayo sanjari na uwepo wa mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Irend, Robbie Keane lakini pia ilishuhudiwa pia na mchezaji wa zamani wa Manchester United na timu hiyo David Beckham.
Steven Gerrard alionekana kutokuwa sawa katika dakika za awali za mchezo huo, kutokana na kutokuelewana vyema na wachezaji wenzake ambao ni wapya kwao.
Hadi dakika ya 25 Los Angeles Galaxy ya Gerrard ilikua ishakubali goli 2-0 toka kwa San Jose Earthquakes.
Lakini Gerrard alianza kukua kimchezo na kusababisha penati iliyofungwa na nahodha wa timu yake mpya, Robbie Keane dakika ya 30.
Dakika saba baadae Gerrard mwenyewe aliisawazishia timu yake na kufanya matokeo kuwa ni 2-2. Gerrard alikimbia hadi kwa mashabiki wake wapya ambao walikuwa wakimshangilia sana.
Akiwa katika uwezo wake tunaoufahamu, Gerrard alifunga tena goli ambalo mwamuzi aliamuru iwekwe penati na kumfanya Robbie Keane afunge hat-trick.
Steven Gerrard alifanyiwa 'sub' katika dakika ya 73 huku akiaga katika pande zote nne za uwanja ambapo mashabiki walisimama kumshangilia.
Gerrard ambaye pamoja na kuvalia jezi namba 8 mgongoni, safari hii alichezeshwa namba kumi, nyuma ya Robbie Keane.
Hadi mechi inaisha pamoja na kuwa nyuma kwa magoli 2-0 ndani ya dakika 25 za mwanzo kutoka kwa San Jose Earthquakes, LA Galaxy walishinda kwa jumla ya magoli 5-2.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video