Mabingwa wa Tanzania bara, Yanga wamepigwa magoli 2-1 na Gor Mahia ya Kenya katika mechi ya ufunguzi ya kombe la Kagame iliyopigwa jioni ya leo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Hata hivyo ukiangalia rekodi ya Yanga kwenye michuano hii, wapinzani wanaweza kuhofia.
Hebu angalia Historia hii....
Mwaka 1993: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni Uganda, mechi ya kwanza Yanga ilifungwa 3-1 na wenyeji SC Villa na ikakutana nao fainali wakawapiga 2 - 1, ndoo ikatua Jangwani.
Mwaka 1999: Wenyeji wa Kagame Cup wakiwa ni wale wale Uganda, mechi ya kwanza Yanga ilifungwa na Rayon Sports ya Rwanda mabao 3 - 0, ikaingia fainali na SC Villa na na kushinda kwa penati, shujaa akiwa ni Peter Manyika Sr. (Baba yake huyu kipa wa Simba SC)

Mwaka 2011: Tanzania wakiwa wenyeji wa Kagame Cup, mechi ya kwanza wakatoa sare ya 2 - 2 na vigogo El Merreikh ya Sudan, tena magoli manne walifunga wachezaji wa El Merreikh. Fainali wakaingia na Simba Feki na kuwafunga goli 1 - 0, bao la Asamoah kufuatia krosi ya Kigi Makassy.
Mwaka 2012: Tanzania wakiwa wenyeji kwa mwaka wa pili mfululizo, mechi ya kwanza ikapigwa 2 - 0 na Atletico ya Burundi, Kavumbagu akiwa na timu hiyo akitupia. Fainali ikaingia na Azam FC na kuwachapa mabao 2 - 0. Magoli ya Hamis Kiiza na Said Bahanuzi
Mwaka huu 2015: Tanzania wenyeji tena, mechi ya kwanza leo Yanga imefungwa 2 - 1 na Gor Mahia ya Kenya.
Je, Historia hii itajirudia?
0 comments:
Post a Comment