Gwiji wa Brazil, Pele amelazwa tena Hospitali kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi nane.
Mwanasoka huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 74 alilazwa kwa wiki mbili mwezi Desemba na kufanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo mwezi Mei katika hospitali ya mjini Sau Paulo.
Mirtes Bogea, afisa habari wa Hospitali ya Albert Einstein amethibitisha kwamba Pele 'Mfalme wa soka' amelazwa Hospitalini hapo siku ya Alhamis kutibiwa tatizo lake la kibofu, lakini hajatoa taarifa zaidi.
0 comments:
Post a Comment