Uchaguzi umeanza kwenye uwanja wa Nou Camp kumpata Rais mpya wa Barcelona huku nahodha wa mabingwa hao wa Ulaya Andres Iniesta akiongoza wachezaji wa zamani na wa sasa kupiga kura kwenye kinyang’anyiro hicho ambacho Josep Bartomeu anapewa nafasi kubwa ya kuibuka na ushindi.
Wachezaji wa zamani na mahodha wa klabu hiyo kwa nyakati tofauti Carles Puyol na Xavi walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kupiga kura ili kuiweka klabu yao kwenye mikono salama.
Josep Bartomeu ni mgombea ambaye anapewa nafasi kubwa ya kuwa rais wa Barcelona lakini anapata upinzani mkali kutoka Joan Laporta, Austi Benedito pamoja na Toni Freixa.
Bartomeu anaonekana kuwa ni chaguo la Luis Enrique (kocha wa Barcelona) baada ya kupewa mkataba mpya na rais huyo wakati yupo madarakani kabla hajaachia ngazi kupisha taratibu za uchaguzi ziendelee mwashoni mwa msimu huu.
Laporta ndiye anaedaiwa kuwa ndiye rais bora kuwahi kutokea kwenye klabu hiyo kati ya mwaka 2003 hadi 2010 kipindi ambacho Barcelona ilishinda mataji mawili ya Ulaya (UEFA Champions League).
0 comments:
Post a Comment