Michael Olunga
SIKu chache baada ya kuichachafya Yanga SC katika mechi ya ufunguzi ya kombe la Kagame iliyochezwa uwanja wa Taifa Dar es salaam, mshambuliaji wa Gor Mahia aliyefunga goli moja katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Wanajangwani ameingia kwenye rada za Simba SC.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe amethibitisha kuanza mazungumzo ya kumsajili Olunga ambaye amekuwa gumzo hapa mjini.
Poppe amesema Olunga ameonekana kuwa mchezaji mzuri, hivyo wanaanza mapambano ya kumtuliza Msimbazi majira haya ya kiangazi.
"Kuna watu wameanza mazungumzo ya awali na Olunga (Michael), mimi bado sijaingia. Sijapata ripoti yoyote kwasababu jana ndio wameanza mazungumzo.
Kenya hawazidi dola 20,000, labda kama amepata ofa sehemu nyingine" Amesema Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment